Social Channels :

 • facebook-32px
 • rss-32px

Events & Updates

Events & Updates - Dar es Salaam Calvary Temple
Sunday, 19 April 2015 03:49

MATANGAZO - April 19, 2015

 1. Tunawakaribisha wageni waliotutembelea na kuabudu pamoja nasi. Karibuni sana DCT.
 2. Kanisa la DCT limeandaa mkutano mkubwa wa Injili katka uwanja wa Shule ya msingi Tabata kuanzia tarehe 27-31/05/2015. Mhubiri wa Kimataifa EV. DALE kutoka Marekani atahubiri. Tujipange vizuri kufanikisha.
 3. Tunahimizwa kulipa ahadi zetu kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kanisa. Gari litawasili bandarini hivi karibuni!
 4. Tangazo la ndoa kwa mara ya kwanza kati ya Eliya Allen Mshiu wa DCT na Odetha Francis wa Kinyerezi. Ndoa yao itafungwa tarehe 10/05/2015 katika kanisa la DCT Tabata
 5. Tangazo la ndoa kwa mara ya pili kati ya Eliya Amos Chavala wa TAG Chumbageni Tanga na Elizabeth Saroy wa Tabata DCT. Ndoa yao itafungwa tarehe 02/05/2015 katika kanisa la DCT Tabata
 6. Jumapili ijayo kutakuwa na tangazo rasmi la uchumba kati ya Jonathan Seni na Theresia Mwanga.
 7. Vijana wote mnaombwa kubaki kwa muda mfupi sana baada ya ibada. Kuna mambo muhimu ya kushirikishwa pamoja na kupokea taarifa ya HARAMBEE kutoka kwa viongozi.
 8. Ibada ya Ushemasi wa Mandela Road (Riverside hadi Tazara, Ilala hadi Mchikichini) itafanyika leo Jumapili kuanzia saa 11 kamili jioni kwa Mama James, (Tabata Matumbi nyuma ya Access Bank, kwenye njia ya Transfoma ya TANESCO, nyumba ya pili yenye geti jeusi. Au piga simu 0718 247 620 – Shemasi.
 9. Washirika wote wanaoishi maeneo ya Mtambani na Msimbazi yote mnaombwa kubaki baada ya ibada wamuone Shemasi Mama Deborah
 10. Zamu za Wiki:
  • Mchungaji: Eresh Tchakubuta
  • Usafi: Wamama (WWK)
  • Uimbaji: New Calvary na Victory Choir.
Published in Events & Updates
You are here: Home Events & Updates Items filtered by date: April 2015